Kiswahili

Karibu!

Urafiki wa Potsdam na Zanzibar; huu ni ushirikiano wa kirafiki kati ya Mji wa Potsdam na Zanzibar.

Uzinduzi wa ushirikiano huu ulifanyika mnamo tarehe 24 Februari 2017 ambapo zaidi ya watu 60  walihudhuria.

Ushirikiano huu unatokana na Mpango wa Asasi za kiraia wa mwaka 2006 ambao ulielekeza kuwa na mashirikiano baina ya Miji ya Kaskazini na Kusini; baada ya mchakato wa kutafuta ni Mji gani unafaa kuwa na mahusiano na Potsdam, na ndipo kwa njia ya kidemokrasia Mji wa Zanzibar ulipendekezwa kuwa mshirika wa Potsdam.

Vilevile mpango huu ulianzishwa kwa sababu Mji wa Potsdam ni mhusika wa uwajibikaji wa Ulimwengu; hivyo basi Mji wa Potsdam unafaa kutoweka mipaka na masharti ya ushirikiano na Miji mengine ya Ulaya na Marekani. Adhma hii ilithibitishwa na azimio la Baraza la Mji wa Potsdam.

Tangu wakati huo, vyama na taasisi mbali mbali za Potsdam zimeanzisha mawasiliano na wenzao wa Mji wa Zanzibar na kupelekea kuanzishwa na kutekelezwa miradi mbali mbali. Kwa mfano mashirikiano kati ya Tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (Zanzibar International Film Festival, ZIFF), ziara za kimichezo kwa timu ya Wanawake wa  mpira wa miguu (Zanzibar soccer queen) kwenda Potsdam.

Mnamo mwaka 2011, kumeanzishwa ushirikiano wa ‘Hali ya Hewa‘ (Climate Partnership) baina ya Potsdam na Zanzibar, miradi mbali mbali imeanzishwa na kutekelezwa kwenye eneo hili.

Mwaka 2014, ujumbe wa kwanza kutoka Potsdam uliongozwa na Mheshimiwa Meya Jahn Jakob uliwasili Zanzibar, katika ujumbe huo taasisi mbali mbali kutoka Potsdam zilishiriki, mfano wa taasisi hizo ni IHK Potsdam, Kiliniki, Shule na vyuo vikuu.

Baraza la Mji wa Potsdam liliidhinisha ushirikiano huo mnamo tarehe 2 Novemba, 2016 baada wenzao wa Zanzibar kuridhia.

Lengo la Urafiki wa Potsdam na  Zanzibar ni kukuza uhusiano wa wahusika wa pande zote mbili, kupeana habari na taarifa za kawaida zinazohusu miradi inayotekelezwa na kupanga shughuli zao kwa pamoja.

Urafiki wa Potsdam na Zanzibar kwa upande wa Potsdam unafanya juhudi kwa kukusanya maoni kwa Umma kuhusu ushirikiano wa pande hizi mbili na kuyafanyia kazi.

Urafiki wa Potsdam na Zanzibar pia unasimamia mawasiliano kati ya Mashirika, taasisi na raia baina ya Miji hii (Potsdam na Zanzibar). Pia huandaa mikutano kwa viongozi wa Miji hii (Mameya) pamoja na viongozi wengine.

Wasemaji wa Urafiki wa Potsdam na Zanzibar ni Cordine Lippert na Kilian Kindelberger, ambao  wanafanya kazi hii kupitia mwavuli wa BBAG e.V.